MUHAS NEWS POST

MAKAMU MKUU WA CHUO AFUNGUA RASMI KAMBI YA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO

 

 

 

 

Katika juhudi za kuimarisha huduma za afya kwa jamii, kuongeza uelewa kuhusu magonjwa ya moyo, na kuelekea uzinduzi wa awamu ya pili ya Kituo cha Umahiri wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Damu, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimefanya ufunguzi rasmi wa Kambi ya Uchunguzi wa Moyo leo tarehe 21 Mei 2025 katika Kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi huo, Makamu Mkuu wa Chuo cha MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa, alisema kuwa lengo la kambi hiyo ni kutoa huduma za uchunguzi wa awali wa magonjwa ya moyo, ambayo yanaendelea kuongezeka nchini kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha.

“Tunawahimiza wananchi wajitokeze kwa wingi kufanyiwa uchunguzi, kwani ugonjwa wa moyo unaweza kukingwa na kutibiwa mapema iwapo utagundulika mapema,” alisema Prof. Kamuhabwa.

Kwa upande wake, Prof. Enica Richard, Mwenyekiti wa Maandalizi ya kambi hiyo, alieleza kuwa timu ya wataalamu kutoka MUHAS imejipanga kikamilifu katika vitengo vyote ili kutoa huduma ya uchunguzi wa awali pamoja na elimu kuhusu magonjwa ya moyo, afya ya moyo, na matumizi sahihi ya dawa zinazohusiana na magonjwa hayo.

Kambi hiyo itadumu kwa siku mbili, kuanzia tarehe 21 hadi 22 Mei 2025, na huduma zinazotolewa ni pamoja na uchunguzi wa moyo

 

 

Facebook
Twitter
LinkedIn