Chuo kikuu cha Afya na Sayansi shirikishi Muhimbili (MUHAS) kwa kushirikiana na Taasisi kutoka Ujerumani Fact Finding Mission wamekutana na kufanya mazungumzo ya namna ya kuwasaidia vijana wa kike wenye mahitaji maalumu kuweza kusomea taaluma mbalimbali za upasuaji yaani (surgery).
Lengo la Kikao hicho kilikuwa ni kujadili maeneo ya kuanzisha ushirikaiano kati ya Ujerumani, Malawi na Tanzania kupitia (MUHAS) kwa kuandika maombi ya ruzuku kupitia DAAD kwa pamoja ili kupata msaada utakaosaidia kuleta mazingira wezeshi kwa wanafunzi wakike wenye uhitaji maalumu kuweza kusomea taaluma mbali mbali za upasuaji yaani (surgery)
Akitoa ushuhuda katika kikao hicho Prof Thomas Kipapa ambaye ni mzaliwa wa Malawi ameeleza jinsi yeye mwenyewe alivyoleta mabadiliko chanya kwenye chuo alichosoma licha ya changamoto ya miguu aliyonayo na hadi sasa ameweza kufanya upasuaji wa ubongo na kichwa kwa zaidi ya wagonjwa 3000 huko ujerumani.
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Prof. Emmanuel Balandya Makamu mkuu wa chuo akitoa neno la shukrani amepongeza hatua hii na kuweka mikakati itakayosaidia kupata watu kutoka MUHAS na MNH pamoja na uanzishwaji wa hati ya makubaliano ( MoU) kati ya pande zote tatu ili kuanza michakato na uhusishaji wa sekta mbalimbali ili kuleta matokeo lengwa katika mahusiano hayo.
Kikao hicho kikiongozwa na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Prof Emmanuel Balandya ,Kaimu,Rasi Ndaki ya tiba (Prof Enica Richard),Akidi Skuli ya Tiba (Dr Peter Wangwe),mkuu wa kitengo cha jinsia (Prof Ester Innocent) pamoja na wawakilishi kutoka idara za upasuaji MUHAS na MNH wakiwa na wawakilishi kutoka Fact Finding Mission Prof Thomas Kapapa ,Neurosurgeon na Mratibu wa Mradi Natascha Ley-Eirish kutoka University Hospital Ulm,Ujerumani.