MUHAS kupitia mradi wa HEET imeandaa warsha ya siku tano ya mafunzo yenye lengo la kuwajengea uwezo Mratibu na wajumbe wa kamati ya dawati la Ukatili wa Kijinsia (Gender Based Violence – GBV Desk) wa kusimamia na kusaidia uanzishaji na uendeshaji wa dawati la Jinsia la Taasisi ya Elimu ya Juu.
Mafunzo hayo yamefanyika kuanzia tarehe 20 hadi 24 Mei 2024 Morogoro na kufunguliwa rasmi na Dkt Rehema Horera (Mratibu wa maswaala ya Jinsia wa mradi wa HEET-Ngazi ya Taifa) kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na wawezeshaji wa mafunzo hayo walitoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Wanawake na Makundi Maalumu na UNICEF.
Akifungua warsha hii, Dr. Horera alieleza kuwa shughuli mbalimbali za masuala jinsia katika mradi ni mojawapo ya mahitaji ya msingi kwa taasisi kuweza kutimiza vigezo vya mradi wa HEET. Dkt Horera pia aliwasilisha mada ya kujenga uelewa wa pamoja kwenye Gender/Sex, Ukatili wa Kijinsia na aina zake.
Akielezea malengo ya warsha hii, Mkuu wa Kitengo cha Jinsia MUHAS na msamamizi wa portfolio ya Jinsia na Elimu Jumuishi wa mradi wa HEET- MUHAS, Dkt Hawa Mbawalla alisema ni kuwaelekeza wanakamati jinsi ya kutumia zana mbalimbali za kuzuia, kushughulikia na kutoa taarifa za GBV/SEA/SH kwa mujibu wa muongozo wa kitaifa na sera na taratibu za MUHAS
Naye mratibu wa dawati la ukatili wa jinsia MUHAS, Prof Ester Innocent ambaye ni Mwenyekiti wa warsha hii alipata nafasi ya kuelezea kwa kifupi Mpango wa Utekelezaji wa Sera ya Jinsia wa mwaka 2023-2026, Sera ya Unyanyasaji wa Kijinsia ya Juni 2023 na Mwongozo wa kuripoti majibu ya GBV katika MUHAS wa Mei, 2024
Katika warsha, hii washiriki walipata fursa ya kujifunza kupitia mada mbalimbali zilizowasilishwa na kusimamiwa na Msimamizi wa madawati la Ukatili wa Kijinsia kwa taasisi za Elimu ya Juu na Kati ngazi ya Taifa na muwezeshaji mkuu wa warsha hiyo, Bi Gift Msowoya.
Baadhi ya masuala yalioyojadiliwa ni pamoja na hongo ya ngono katika vyuo vikuu, usimamizi wa kesi za ukatili wa kijinsia katika vyuo vya elimu ya juu, unyanyasaji mtandaoni, viashiria cha unyanyasaji mtandaoni na kupata maelezo kuhusu kitabu cha usajili cha Dawati la Jinsia na mifumo ya kuripoti. Warsha
Washiriki pia waliweza kuandaa mpango kazi wa utekelezaji wa Sera ya ukatili Jinsia wa mwaka 2023-2026 wa MUHAS na utaratibu wa uendeshaji wa matukio ya ukatili wa jinsia (GBV- standard operating procedures).