Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili ( MUHAS) Bi. Marsha Macatta- Yambi pamoja na wajumbe wa Baraza hilo wametembelea miradi ya ujenzi ambayo chuo inaendelea kutekeleza kupitia mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi ( HEET) katika Kampasi ya Mloganzila.
Lengo la ziara hiyo ni kutathmini maendeleo ya miradi hiyo, kuhakikisha inakamilika kwa wakati na utekelezaji wake unafuata viwango vilivyowekwa na vinaendana na malengo ya taasisi.
Kaimu Mwenyekiti pamoja na wajumbe wa baraza hilo walitembelea mradi wa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi, madarasa ya kufundishia, Maabara ya kisasa, Maktaba, jengo la utawala na ujenzi wa Ndaki ya Tiba.
Katika ziara hiyo Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Bi. Marsha Macatta- Yambi amewasisitiza wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa majengo hayo kwa wakati kama mkataba unavyoeleza.
Ujenzi wa miradi hii inatarajiwa kumalizika mnamo mwezi Juni 2026 na imekusudiwa kwenda kuimarisha miundombinu ya chuo, kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia, pamoja na kuongeza uwezo wa kudahili wanafunzi wengi zaidi.