MUHAS NEWS POST

MUHAS YAPOKEA GARI LA PILI KUWEZESHA SHUGHULI ZA UTEKELEZAJI WA MRADI WA HEET

Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa akikata utepe kama ishara ya kupokea rasmi gari la kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa HEET

 

Makamu Mkuu wa Chuo na wajumbe wa vitengo vya utekelezaji wa mradi wa HEET wakishangilia mara baada ya kupokea rasmi gari hilo kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za mradi wa HEET.

 

Wajumbe wa Utekelezaji wa Vitengo vya Utekelezaji wa Mradi wa HEET MUHAS katika sherehe fupi ya kupokea gari la mradi iliyofanyika chuoni, MUHAS

 

Gari aina ya Coaster lililopokelewa leo na uongozi wa chuo kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji wa shughuli za HEET

 

Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa akiendesha gari mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) katika utekelezaji wa maeneo saba ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mabadiliko ya Kiuchumi (HEET) kimepokea gari la pili  la aina ya Coaster kati ya magari manne yatakayo nunuliwa na mradi wa HEET kwa lengo la kurahisisha utekelezaji wa shughuli za mradi huo mkubwa ikiwemo ufuatiliaji wa masuala ya ujenzi.

Amebainisha hayo Dkt. Nathanael Sirili Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS wakati akizungumza kwenye sherehe fupi ya kupokea gari hilo chuoni, MUHAS. Dkt. Sirili alieleza kuwa kupitia mpango wa ununuzi wa  shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP), ambao umeweza kupunguza gharama kwa kiasi kikubwa  kutoka  shilingi ya kitanzania milioni 450,000,000 kwa gari la kwanza na la pili hadi shilingi milioni 312,000,000/= na hivyo kuweza kuokoa takribani shilingi milioni 138 za kitanzania kama utaratibu wa kawaida ungetumika.

Dr. Sirili aliongezea kuwa gari hii itatumika kuwapeleka wafanyakazi na wanafunzi kwenye mafunzo kwa njia ya vitendo na hivyo kuimarisha mafunzo na mafungamano ya sekta ya afya na elimu kwa ujumla.

Naye Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Prof. Erasto Mbugi aliwapongeza wajumbe wa kitengo cha utekelezaji wa mradi wa HEET kwa ufanisi mkubwa katika kuhakikisha kinachopangwa ndicho kinazotekelezwa na vilevile alimshukuru Makamu Mkuu wa Chuo kwa kuhakikisha vibali vinatoka kwa kasi na kasi hiyo ndo imeleta matunda ya kupokea gari hili la pili leo.

“Gari hili linatumika katika shughuli zote cha chuo, watekelezaji wa mradi wa HEET wakiwa na shughuli watatumia nia hili ni gari la chuo ambalo limefadhiliwa na mradi wa HEET na taratibu zote za kuliendesha zitafata kama tulivyojiwekea hapa chuoni,” alisema Prof. Mbugi

Akiongea baada ya kupokea na kuzindua gari hilo, Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS Prof. Appolinary Kamuhabwa aliwapongeza wasimamizi wa mradi katika kufanikikisha utekelezaji wa mradi huu kwa kuleta gari la pili.

“Kikubwa hapa tumesikia tumefikisha gari la pili tukiwa tumeokoa kiasi kikubwa cha pesa na kutokana na kuokoa pesa hizo tutaweza kuongeza magari mawili mengine ambayo yatasaidia sana katika mradi na taasisi pia,”alisema Prof. Kamuhabwa.

Aidha Prof. Kamuhabwa  ametoa wito kwa watekelezaji wa mradi huu kuendelea  kufatilia magari mengine mawili ambayo hayajafika na kuhakikisha kuzingatia muongozo wa utunzaji  wa magari haya mapya  unafutatwa ikiwa lengo ni kuyalinda na kuhakikisha tunatekeleza malengo ya mradi ambao ni mahususi kwa ajili ya kuleta mageuzi ya kiuchumi katika Elimu ya juu nchini.

 

Facebook
Twitter
LinkedIn