skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Mratibu wa Mradi wa HEET, MUHAS Prof. Erasto Mbugi akimtambulisha mshauri elekezi kwa wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS katika kikao kilichofanyika kampasi ya Mloganzila
Wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS wakifatilia taarifa ya mshauri elekezi katika kikao.
Mshauri Elekezi kutoka kampuni ya ARQUES AFRICA, Prof. Huba Nguluma ( wa kwanza kulia) akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa majukumu kwa wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS
Wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS na na timu ya Mshauri Elekezi wa masuala ya usanifu na usimamizi wa majengo kutoka ARQUES AFRICA katika kikao cha makabidhiano ya site, Mloganzila
Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET,MUHAS, Dkt. Nathanael Sirili akitoa neno la shukrani wa wajumbe Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS na na timu ya Mshauri Elekezi kabla ya makabidhiano ya site, Mloganzila
Mratibu wa Mradi wa HEET, MUHAS Prof. Erasto Mbugi akiwa na Naibu wa Mradi, Dkt. Nathanael Sirili na Wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS wakikabidhi rasmi site kwa Mshauri Elekezi na Timu yake kwa ajili ya utekelezaji
Makabidhiano ya Site, Mloganzila
Makabidhiano ya Site, Mloganzila

MUHAS WAKABIDHI SITE KWA MSHAURI ELEKEZI WA KAMPUNI YA ARQES AFRICA KAMPASI YA MLOGANZILA

15 DISEMBA 2023

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi, HEET leo kimefanya makabidhiano ya eneo (site) na Mshauri Elekezi kwa ajili ya kuandaa usanifu na usimamizi wa ujenzi wa majengo na miundombinu ya Ndaki ya Tiba katika kampasi ya Mloganzila.

Akizungumza katika kikao cha wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS na timu ya Mshauri Elekezi wa masuala ya usanifu na usimamizi wa majengo kutoka ARQUES AFRICA, Mkuu wa Kitengo cha Manunuzi MUHAS, Bw, Charles Mnyeti amesema kuwa madhumuni ya kikao hiki ni kutambuana na kuwa na uelewa wa pamoja katika kazi inayokwenda kufanyika kupitia mradi huu.

Akielezea majukumu waliopewa katika mradi huu kiongozi Mshauri Elekezi wa Kampuni ya ARQUES AFRICA Prof. Huba Nguluma amesema ni usanifu wa majengo ya Ndaki ya Tiba ikiwa ni pamoja maktaba na TEHAMA, mgahawa wa watumishi na wanafunzi, hosteli za wanafunzi,  Barabara za ndani na miundombimu ya michezo.

Mshauri Elekezi huyo aliongezea kuwa atawasilisha taarifa ya kazi zake ambayo itapitiwa na Kamati ya Menejimeti ya Chuo kwa ajili ya kujiridhisha na hivyo kutoa nafasi ya kutangaza kandarasi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi wa miundombinu tajwa. Pia aliahidi kufanyia kazi mapendekezo yaliyotolewa na kuomba ushirikiano wa karibu na haraka pale utakapohitajika ili kuweza kukamilisha kazi hii mapema iwezekanavyo.

Naye Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET, Dkt. Nathanael Sirili alisisitiza kuzingatia makubaliano ya kwenye mkataba na kuboresha zaidi ili kutimiza kwa wakati utekelelezaji wa mradi huu. “Tuna matumaini na tuna waamini mtafanya kazi kwa kuzingatia muda tuliokubalina. Shauku kubwa ya menejimenti ni kuona hatua ya awali inakamilika mapema ili kutoa nafasi kwa Mkandarasi kuanza kazi mapema”, amesema Dkt. Sirili.

Makabidhiano haya yamefanyika leo tarehe 15 Disemba 2023 na kuhudhuriwa na Mratibu na Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET, MUHAS, wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS na timu ya Mshauri Elekezi wa masuala ya usanifu na usimamizi wa majengo  kutoka ARQUES AFRICA