skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Naibu Mratibu wa Mradi wa HEET, MUHAS, Dkt. Nathanael Sirili akitoa salamu za ukaribisho katika hafla ya utiaji saini mkataba kati ya MUHAS na kampuni ya ARQUES AFRICA
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa na Mshauli Elekezi kutoka kampuni ya ARQUES AFRICA, Prof. Huba Nguluma wakitia saini mkataba wa kuandaa usanifu na usimamizi wa ujenzi wa majengo na miundombinu katika kampasi ya Mloganzila
Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Prof. Appolinary Kamuhabwa na Mshauri Elekezi kutoka Kampuni ya ARQUES AFRICA, Prof. Huba Nguluma wakionyesha mikataba baada ya kumaliza zoezi la kusaini
Mratibu na Naibu Mratibu Mradi wa HEET, MUHAS wakiwa kwenye picha ya pamoja na mshauli Elekezi na wajumbe kitengo cha wajumbe wa Kitengo cha Utekelezaji wa Mradi, PIU MUHAS 

15 Disemba 2023

Katika mwendelezo wa utekelezaji wa mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi “HEET – Project” Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili  kimesaini mkataba na Kampuni ya ARQES AFRICA kwa ajili ya kuandaa usanifu na usimamizi wa ujenzi wa majengo na miundombinu katika kampasi ya Mloganzila .

Akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Appolinary Kamuhabwa amemtaka Mshauri elekezi kukamilisha usanifu wa majengo kwa viwango na wakati na kusimamia ujenzi kwa umakini na kwa kuzingatia thamani ya fedha.

“Natoa wito kwa mshauri elekezi wa kampuni ya ARQES AFRICA kufanya kazi yake kwa uweledi wa hali ya juu ili kazi zote zikamilike kwa ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango”, alisisitiza Prof. Kamuhabwa.

Prof. Kamuhabwa ameongeza kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kampasi ya Mloganzila ni mkakati wa serikali katika kuboresha na kuleta mageuzi ya kiuchumi na miuondombinu katika elimu ya juu na ni miongoni mwa miradi muhimu kitaifa na kimataifa.

Naye Mratibu wa Mradi wa HEET, Prof. Erasto Mbugi amesema hatua hii ni mwendelezo mzuri wa kuhakikisha mradi wa HEET unakamilika kwa ufanisi kama yalivyo malengo ya mradi na taifa kwa ujumla. Ameishukuru Serikali kwa mradi huu ambao ameeleza kuwa una tija kwa Chuo kwa kuwa kupitia mradi wa HEET, MUHAS inaenda kujenga na kuboresha miundombinu, na ndio sehemu ya mkataba uliosainiwa.

Aidha kiongozi wa Mshauri Elekezi wa Kampuni ya ARQUES AFRICA, Prof. Huba Nguluma amekishukuru Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kwa kuwapa fursa ya kufanya kazi kwa pamoja katika kutekeleza mradi wa HEET. Prof Nguluba ameahidi kutekeleza majukumu waliyopewa kwa weledi, ubora na ufanisi mkubwa ili kufikia malengo yao kama kampuni lakini pia kusaidia malengo ya Chuo na Serikali kwa ujumla. Amesisitiza kuwa kampuni yao ina wataalamu wa kutosha kukamilisha kazi kama ilivyopangwa.