skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Prof. Erasto Mbugi akizungumza timu ya wakaguzi kutoka OCAGZ walipotembelea ofisini kwake
Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Prof. Erasto Mbugi, Naibu Mratibu, Dkt Nathanael Sirili na Mwenyekiti wa timu kutoka OCAGZ, Mbaraka Ukasha Habibu wakati wa kikao na baadhi ya wajumbe wa kitengo cha utekelezaji wa mradi wa HEET MUHAS
Timu ya wakaguzi kutoka OCAGZ na mjumbe kutoka SUZA walipotembelea Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS
Timu ya wakaguzi kutoka OCAGZ na mjumbe kutoka SUZA walipotembelea Ofisi ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS
Wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa HEET MUHAS wakiwa katika picha ya pamoja na wakaguzi kutoka OCAGZ baada ya kikao kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa mradi wa HEET

18 Oktoba, 2023

Timu ya wakaguzi kutoka Ofisi ya Mkaguzi wa Ndani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, OCAGZ wametembelea mradi wa HEET MUHAS kwa nia ya kufanya ulinganifu (benchmarking) wa utekelezaji wa mradi.

Akizungumza kutambulisha timu hii ya watu watatu, Msaidizi wa Mratibu wa mradi wa HEET Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), Dkt Haji A. Haji amesema kwamba mradi wa HEET na kwa upande wa Zanzibar unatekelezwa na taasisi moja tu ambayo ni SUZA. Amesema kuwa baada ya utekelezaji wa mradi huu kwa kipindi cha mwaka mmoja SUZA wamepata wakaguzi kutika ofisi ya OCAGZ ambao pamoja na kuwakagua wameona wafanye pia ulinganifu (benchmarking) kwa baadhi ya taasisi ambazo zinatekeleza mradi huu.

Naye Mwenyekiti wa Timu hii Mbaraka Ukasha Habibu amesema timu imetumwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuupitia mradi kisha kuishauri Serikali kwa lengo la kuhakikisha kwamba mradi wa HEET unatekelezwa ipasavyo na kufikia malengo yaliyokusudiwa. Ameongeza kuwa katika miradi ya Chuo huu ni mradi mkubwa ina maana kama utayumba au kama hautujafikia malengo Chuo kitadhirika na Serikali kwa ujumla.

Ameeleza kwamba Chuo cha MUHAS ni miongoni mwa vyuo ambavyo vina muelekeo mmoja na SUZA na hii ina maana kwamba kimpangilio na vitu vingine vitakuwa vinafanana, “Kuja kwetu huku pamoja na mambo mengine ni kuangalia changamoto zilizopo bila shaka kwa namna moja au nyingine zinafanana, sasa vipi mnazitatua au mpaka sasa mmefikia wapi, na sisi tukatumia maarifa yetu na kuweza kutoa ushauri kwa SUZA na kwa serikali kwa ujumla”, aliongeza.

Akiongea katika ugeni, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo, Mipango, Fedha na Utawala ambaye pia ni Mratibu wa Mradi wa HEET MUHAS, Prof. Erasto Mbugi ameeleza kuwa mradi wa HEET MUHAS umefanyiwa ukaguzi wa ndani na wa nje mara kadhaa. Amesema kuwa wakaguzi wanakufumbua macho kwenye vitu ambavyo unaweza ukafanya usijue unafanya kwa usahihi au la.

Amesema kuwa mradi wa HEET una miongozo ya jinsi ya kufanya kazi katika mradi huo. Kwa hiyo watu wanaofanya kazi katika mradi huu wanafanya kwa muongozo ambao wanao. “Kwa hiyo vitu vingi ambavyo labda mnaweza kuona ni namna anatekeleza yale ambayo yameelekezwa”, aliongeza.