skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Mahututi, MUHAS,Dkt. Said Kilindimo akitoa mwenendo wa mafunzo wakati wa sherehe ya kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika chuoni, MUHAS
Mkuu wa Skuli ya Sayansi ya Tiba, MUHAS, Dkt. Peter Wangwe akitoa salamu za ukaribisho katika sherehe za kufunga mafunzo ya watoa huduma wa afya katika idara ya magonjwa ya dharura na mahututi
Mgeni rasmi, Bw. Raymond Kiwesa akifunga rasmi mafunzo ya watoa huduma yaliyofanyika chuoni, MUHAS.
Watoa huduma wa afya wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi
Watoa huduma wa afya wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi
Watoa huduma wa afya wakifatilia hotuba ya mgeni rasmi
Mshiriki wa mafunzo akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo yaliyofanyika chuoni, MUHAS.
Mshiriki wa mafunzo akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo yaliyofanyika chuoni, MUHAS.
Mshiriki wa mafunzo akipokea cheti baada ya kuhitimu mafunzo yaliyofanyika chuoni, MUHAS.
Mkurugenzi wa kozi, Prof. Hendry Sawe akitoa neno la shukrani wakati wa sherehe za kufunga mafunzo ya watoa huduma wa afya yaliyofanyika chuoni, MUHAS
Mgeni rasmi, Bw. Raymond Kiwesa akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji na kamati ya maandalizi ya mafunzo mara baada ya kufunga rasmi mafunzo hayo.
Mgeni rasmi, Bw. Raymond Kiwesa akiwa kwenye picha ya pamoja na wawezeshaji, kamati ya maandalizi na washirki wa mafunzo mara baada ya kukabidhiwa vyeti.

08 Septemba 2023

Naibu Katibu Mkuu Afya- TAMISEMI aliyewakilishwa na Afisa wa afya, Bw. Raymond Kiwesa Leo tarehe 08 septemba, 2023 amefunga rasmi mafunzo ya huduma kwa wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi kwa watumishi wa afya kwa hospitali za wilaya. Mafunzo hayo yaliyoendeshwa kuanzia mwezi Juni 19 hadi Septemba 08, 2023 kwa kushirikiana ofisi ya Rais- TAMISEMI na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili. 

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Afisa Afya, Bw. Raymond Kiwesa aliwasisitiza watumishi wa afya kuwahudumia wananchi kwa weledi na ubora zaidi kwa sababu mafunzo haya yamelenga kuimarisha huduma za afya zinazotolewa hasa katika idara kuhudumia wagonjwa wa Dharura na Mahututi 

Bw. Kiwesa  aliongezea kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi sana katika vifaa na ujenzi wa majengo ya dharura na wagonjwa mahututi katika ngazi ya Hospitali ya Wilaya kwa lengo la kusongeza huduma hizi karibu zaidi na wananchi.

“Ni mategemeo ya Serikali kwamba kupitia mafunzo haya watumishi wetu wamejengewa uwezo wa kwenda kutoa huduma bora kwa wananchi na serikali itahakikisha inaendelea kuweka mazingira mazuri ya kutolea huduma katika vituo vyenu”, alisema Bw. Raymond

Kwa upande wake Mkuu wa Idara Magonjwa wa dharura na Mahututi kutoka MUHAS, Dkt. Said Kilindimo alisema mafunzo haya yalitolewa katika makundi matano kutoka Hospitali za Muhimbili, Bugando, KCMC, Benjamini na Mbeya. Na watumishi 538 walipata mafunzo kwa njia ya mtandao na watumishi 477 walipata mafunzo ya ana kwa ana na kati ya hao watumishi 473 walihitimu na kufaulu vizuri. 

Dkt. Said alishukuru juhudi za serikali kupitia ofisi ya Rais- TAMISEMI  kwa kuwezesha mafunzo hayo na alipendekeza kuwa mafunzo haya yawe endelevu ili kuwawezesha watoa huduma za afya katika maeneo yao ya kazi hasa kwenye idara ya magonjwa ya dharura na mahututi.

Naye Mkuu wa Skuli ya sayansi ya tiba, MUHAS.Dkt. Peter Wangwe aliwasihi washiriki waliopata fursa ya kupata mafunzo hayo watumie ujuzi huo vizuri na kuwa mstari wa mbele katika kuokoa maisha ya watanzania na kufanya kazi kwa weledi na kwa hali ya juu pamoja na kuhakikisha wanakuwa wakufunzi kwa watoa huduma wengine wa afya katika maeneo ya kazi.