Matukio katika Picha: Wananchi wakijione bunifu mbalimbali zilizofanywa na wataalamu kutoka MUHAS kwenye Maonesho ya Wiki ya Ubunifu katika Uwanja wa Jamhuri, Dodoma








Chuo Kikuu cha Afya na Sayanshi Shirikishi., Muhimbili washiriki Maonesho ya Wiki ya Ubunifu Kitaifa yalioandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Katika Maonesho hayo MUHAS wanaonesha bunifu mbalimbali zilizofanywa na wataalamu kutoka Chuoni hapo. Bunifu hizo ni SKYMED App ni app ambayo inatumia akili bandia kuunganisha watu na wataalamu wa afya, Afya AI ni app ambayo hutumia akili bandia kutambua hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari na presha, MIA sanitizer ni sanitizer ya kupuliza yenye kemikali kutoka kwenye mimea iliyo na uwezo maradufu wa kuua na kusambaa zaidi, Mti wa Mlonge katika kuongeza mnyororo wa thamani wa mbegu za Moringa Oleifera kwa kutibu maji kwenye jamii zilizokumbwa na ukame, na ya mwisho ni bunifu ya kifaa cha Salimeter chenye uwezo wa kupima wingi wa chumvi kwenye chakula ili kupunguza magonjwa yamoyo na shinikizo la damu.
Maonesho haya yameanza tarehe 24 Aprili katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma na yanatarajiwa kufungwa siku ya ijumaa tarehe 28 Aprili 2023.