skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Prof. Andrea Pembe akitoa neno la ukaribisho wakati wa kongamano la kusambaza matokeo ya tafiti za Uviko 19 iliyofanyika chuoni, MUHAS
Washiriki wakifatilia hotuba inayotolewa na Makamu Mkuu wa Chuo, MUHAS (haonekani kwenye picha) wakati wa ufunguzi wa kongamano
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akifungua kongamano la kusambaza matokeo ya tafiti za Uviko 19 iliyofanyika chuoni, MUHAS
Washiriki wakifatilia hotuba inayotolewa na Rais Mwinyi wakati wa ufunguzi wa kongamano la kusambaza matokeo ya tafiti za Uviko 19 iliyofanyika chuoni, MUHAS
Bw. Ahmed Salim, mtoto wa Amne Salim ambaye alikuwa mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania akitoa neno la shukrani wakati wa ufunguzi wa kongamano
Prof. Eligius Lyamuya kutoka Idara ya Immunolojia na Microbiolojia akilelezea Mlipuko, Mabadiliko,
Hatua za Kukabili na Tuliyojifunza kipindi cha mlipuko wa Uviko 19
Mmoja wa Mtafiti, Prof. Karim Manji akielezea matokeo ya tafiti ya uenezi wa viashiria vya kinga dhidi ya Uviko 19 kwa wakina mama walioko kwenye umri wa kuzaa
Mmoja wa Mtafiti, Ms. Leonida Simon akielezea matokeo ya tafiti kuhusu dhana na mtazamo wa chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa watu wazima katika wil;aya ya Ilala, Moshi na Kirimanjaro

Jumanne, Machi, 17

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewapongeza wanasayansi wa MUHAS kwa kazi nzuri wanayoifanya kwenye tafiti na machapisho.  Ameyasema hayo leo wakati wa akifungua Kongamano la Kusambaza Matokeo ya Tafiti za Uviko-19 zilizofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili kwa ufadhili wa familia ya Amne Salim.

Akizungumza katika kongamano hilo, Dkt. Hussein Mwinyi amesema, MUHAS imekuwa mstari wa mbele katika tafiti kutatua changamoto zinazotukabili ili kuleta unafuu kwa raia wa Tanzania na kuweza kufikia malengo endelevu tuliyojipangia.

Alisisitiza kuwa Taifa bora hujengwa na raia wenye afya na lengo hili litafikiwa kwa kufanya tafiti zinazotatua changamoto za wananchi na kutoa ushauri wa kitaalamu kupitia tafiti hizo. “Serikali yenu ipo nyuma yenu katika kuhakikisha mnafikia malengo hayo. Hongereni sana”, aliongeza Rais Mwinyi.

Rais Mwinyi pia aliwapongeza MUHAS kwa uwazi, weledi, na utendaji adilifu katika utekelezaji wa ufadhili wa Amne Salim. Amesema kwamba Chuo kimeutendea haki ufadhili huu kwa kuishirikisha familia katika hatua zote na kufikia kwa pamoja malengo ya ufadhili huu.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda alitoa shukrani zake za pekee kwa familia ya Amne Salim kwa ufadhili wa kuendeleza tafiti hapa chuoni. Waziri pia alitoa wito kwa wadau mbalimbali kuungana na serikali katika kuwezesha tafiti za sayansi hasa maeneo ya tiba. “Kwa sababu tusipofanya mambo kwa utafiti tutakuwa tunacheza mazingaombwe na haitatupeleka popote, hatuwezi kufanya pata potea kwenye maisha ya watu”, aliongeza Prof. Mkenda

Aidha kwa kuzingatia hilo Waziri alisema kuwa Serikali imetenga fedha kwa watafiti wa vyuo vikuu vya Tanzania ambao wataweza kuchapisha matokeo ya tafiti zao katika majarida ya juu kabisa duniani ambacho ni kigezo cha kuonyesha umuhimu na faida ya utafiti wao. Kila mtafiti atakayeweza kufanya hiyo atapewa shilingi milioni 50.

Akiongelea takwimu za kazi za tafiti Chuoni, Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Andrea Pembe amesema tafiti hizi zimeweza kusambazwa kwenye majarida ya kisayansi (scientific journals) na kufikia 450-500 kwa mwaka na kutengenezewa mihtasari ya sera (policy briefs) na vile vile na kuandaa mijadala ya kitaalamu iliyobadili utendaji na utoaji huduma za afya nchini.

“Hivyo basi siwezi kuishukuru vya kutosha familia ya Amne Salim kwa uamuzi huu wa kushirikiana nasi kwenye masuala ya utafiti. Ni matumani yetu kwamba kwa mfano huo ambao familia ya Amne Salim imeuweka, taasisi, mashirika na watu binafsi nchini wataguswa na kuona umuhimu wa kushirikiana nasi katika masuala ya tafiti za afya nchini”, alisema Prof. Andrea Pembe.

Naye, mtoto wa Amne Salim ambaye alikuwa mke wa Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Salim Ahmed Salim, Bw. Ahmed Salim, amesema sababu za kuanzisha mfuko huo ni katika kusaidia jamii kukabiliana na ugonjwa wa COVID 19 ambao umesababisha vifo vya watu wengi ikiwemo mama yao, Amne.

Amesema ugonjwa huo umekuwa na athari kubwa kwa familia nyingi nchini Tanzania na duniani na kwamba utafiti wa kisayansi utasaidia katika kutoa taarifa sahihi kuhusu ugonjwa huo ikiwemo tabia, maambukizi na namna ya jamii kujikinga

“Baada ya mama yetu kufariki dunia sisi kama familia tulikaa na kuona ni namna gani tutachangia katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu na namna ambayo watanzania wataweza kunufaika na fedha tutakazozitoa”, alisema Ahmed.

Katika Kongamano hili tafiti nane ziliweza kuwasilishwa na watafiti kutoka MUHAS, tafiti hizo ni uenezi wa viashiria vya kinga dhidi ya virusi vya Uviko19 kwa waakina mama walioko kwenye umri wa kuzaa, Afya ya akili na visababishi vyake kwa wafanyakazi wa afya wakati wa mlipuko wa Uviko 19 na Hofu na Kusita kupata chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa wamama wajawazito walioudhuria kliniki na

Nyingine zilikuwa ni Kushawishi kuhusu chanjo dhidi ya Uviko 19 kuna budi kuchunguza dhana zilizo leo, Dhana na mitazamo kuhusu chanjo dhidi ya Uviko 19 kwa watu wazima wilaya ya Ilala, Moshi na Kirimanjaro, kuchunguza uzoefu wa jamii katika kutumia dawa za asili wakati wa Uviko 19, Uchunguzi wa kinga ya mwili baada ya maambukizi na baada ya chanjo, na dalili za Uviko 19 kwa watoto.