skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili Katika Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia katika sherehe za kufunga maonyesho hayo yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael na Mwenyekiti wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania Prof. Penina Muhando wakipata maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na MUHAS kutoka kwa Afisa Habari na Mawasiliano (MUHAS), Bi. Neema Edwin wakati walipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili kwenye maonesho ya 17 Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Maonesho hayo yamefungwa leo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili, Prof. Andrea B. Pembe akitoa maelezo kuhusiana na tafiti na dawa za asili zinazotengenezwa na Taasisi ya Dawa ya Asili Muhimbili kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia alipotembelea Banda la MUHAS kwenye Maonesho ya 17 Ya Elimuya Juu yalioandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Francis Michael akipokea zawadi wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili kwenye Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia yalioandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, mhe. Francis Michael ametembelea banda la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili katika Maonyesho ya 17 ya Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na MUHAS wakati wa sherehe za kufunga maonesho hayo tarehe 23 Julai 2022.

Katika Banda la MUHAS, Katibu Mkuu aliweza kufahamu programu mbalimbali zinazotolewa na Chuo kuanzia ngazi ya Diploma mpaka uzamivu Na kufahamu tafiti na madawa ya asili yanayotengenezwa na wataalamu kutoka Taasisi ya dawa ya asili Muhimbili.

Maonyesho hayo yaliondaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ( TCU) yamefungwa rasmi leo tarehe 23 Julai 2022 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja