skip to Main Content
P.O. Box 65001, MUHAS,Dar es Salaam webmaster@muhas.ac.tz 0752360543 / 0756265177 - Admission Office

PICHA : Watumishi wa MUHAS wakifanya usafi nje ya jengo la Kinywa na Meno katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma

21 Juni, 2022

Katika kuadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma watumishi wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi, Muhimbili wamefanya usafi wa mazingira nje ya  jengo la Skuli   ya Kinywa na Meno lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Akizungumza katika zoezi hilo la usafi, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Utawala katika Kurugenzi ya Rasilimali watu,MUHAS  Bi. Sarah Kijuu amesema moja ya jukumu ambalo tumepewa katika kuadhimisha hii wiki ya utumishi wa umma ni kufanya shughuli za kijamii katika maeneo ambayo wananchi wanapata huduma.

“Leo tumefika hapa kufanya usafi nje ya jengo la Skuli ya  Kinywa na Meno  ambayo  ni skuli   moja wapo hapa MUHAS inayotoa huduma ya kijamii katika matibabu ya Kinywa na meno.Na huu ni muendelezo wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma yalioanza   tarehe 16 mpaka 23 Juni 2022”,Alisema Bi. Sarah.

Vile Vile aliwashukuru watumishi wa MUHAS waliojitokeza katika zoezi la kufanya usafi  nakutoa wito kwa watumishi wengine kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho yajayo.

Kauli ya mbiu ya mwaka huu ni Nafasi ya Mapinduzi ya Nne ya Viwanda katika masuala mapya yanayojitokeza kuhusu utoaji wa huduma na urejeshaji wakati na baada ya janga la Corona.