MUHAS kupitia kitengo cha Programu ya Jinsia ( Gender Program Unit) wamefanya semina ya mwongozo wa fani za afya na Sayansi Shirikishi kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari wilaya ya Ilala.
Kupitia semina hiyo wanafunzi waliwenza kupata fursa ya kujua programu mbalimbali za afya zinazotolewa MUHAS na vigenzo vyake kuanzia ngazi ya Diploma mpaka Digrii.
Pia Mkuu wa Kitengo cha Programu ya Jinsia Dkt. Hawa Mbawala aliwapatia elimu na muongozo wa kufia ndoto za kuwa madaktari, wauguzi, wafamasia, wataalamu wa elimu ya jamii.
Mafunzo hao yaliweza kuhudhuriwa na wanafunzim kutoka Kisutu, Jangwani, Tambaza, Benjamini Mkapa, Tusiime na Almuntazir.




