Mwakilishi wa Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Ayoub Kibao, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi na Mkuu wa Idara ya Tiba wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) ambaye pia ni Mkuu wa Utafiti katika programu ya sikoseli na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo, Paschal Ruggajo wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kliniki maalum ya wagonjwa wenye sikoseli ambao pia wanakabiliwa na magonjwa ya moyo iliyoko katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete jijini Dar es Salaam.